Vipo vitu vingi ambavyo watu tunavifanya pasipo kujua faida na hasara yakufanya vitu hivyo japo wakati mwingine si vyema kuangalia sana upande wa hasara unapofanya kitu fulani, wenzetu wanasema "negative minds will never produce +ve things."
Kama nilivyosema vipo vitu vingi lakini kwa Leo tazungumzia kitu kimoja kitakachofuatiwa na vitu vingine vingi kwa siku nyingine. Kitu hiki ni *SOCIAL NETWORKS RELATIONSHIPS*
Matangazo ya husiano katika mitandao ya kijamii. Si vibaya wala dhambi kumtambulisha Yule umpendae kwa dhati katika mitandao ya kijamii tena inaweza kuwa vizuri zaidi kuliko vibaya kwakuwa mipaka ya watu wengine kwa huyo umpendae kwa dhati inawezakuwa mikubwa kwaajili yakulinda mahusiano yenu.
Lakini hakuna kitu chenye faida kisicho na hasara, hasara yakufanya hivyo naamini tunazijua ila naweza tu kuikumbushia moja. Hasara inakuja pale migogoro inapoibuka katika mahusiano na wakati mwingine mahusiano kuvunjika kabisa! Kweri inaumiza sana kwasababu hapo ndipo utakapoiona hasara ya huo mtandao wako uliokuwa ukiutumia kuwaonesha watu ni jinsi gani ulikuwa unampenda kwa dhati huyo mwenzi wako.
USHAURI
Mimi na wewe tuwe makini katika matumizi ya mitandao yetu ya kijamii tunayoipenda sana sana kwasababu kuna Leo na kesho, kwa hakika hatuwezi fahamu kitatokea nini. Hivyo basi ili kuepuka kumuumiza mtu au kuumizwa au kuumizana kupitia mitandao kitu chakwanza kabisa nikuwa makini na kitu unachopost, au huyo unaemtambulisha kwa umma! Je huyo unaempost kwa Upendo wako wa dhati kutoka moyoni na sehemu zote za mwili wako anautambua uepo wako katika maisha yake? Kama anautambua basi kunavitu ambavyo hakika ni yeye atakaesaidia huo mtandao wakijamii usionekane mchungu kwako mbele ya wanajamii hata endapo utatokea mgogoro wa aina yoyote katika mahusiano yenu.
Sina mengi, Mwenyezi Mungu akijaalia tutaendelea kupeana mengine mengi na mazuri zaidi. Maoni, ushauri na mchango wako wowote kuhusiana na hili jambo kadili mwenyezi Mungu alivyokuongoza niwamuhimu na unakaribiswa sana.